VIJANA wenye vipaji vya sanaa wameshauriwa kujiunga na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ambako kuna wataalam wabobezi katika maswala ya sanaa ili waweze kupata ujuzi kwa kufundishwa mbinu mbalimbali na kuwa wasanii bora zaidi.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Herbert Makoye leo April 29, 2023 wakati akizungumza katika kipindi cha Baragumu Live kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Channel ten.
Dkt. Makoye amesema mafunzo ni muhimu sana kwa wasanii kwa kuwa yanawapa fursa ya kufanya vitu tofauti kulingana na vipaji vyao tofauti na wasanii ambao hawakupita darasani.
"Elimu hii ya sanaa ambayo inapatikana TaSUBa inamfanya msanii ajitambue na atambue mazingira ya kazi yake hivyo kutoa kazi zilizo bora," amesema Dkt. Makoye.
Mkuu huyo wa TaSUBa ameongeza kuwa elimu inapanua na kuboresha pale msanii alipo na kwenda mbele zaidi akielewa kwamba siku zote elimu haimrudishi mtu nyuma bali inamuongezea zaidi.
Dkt. Makoye amewashauri wasanii wenye vipaji kuwa ni vizuri kipaji kikaboreshwa na wataalam kwa kwenda Chuo kusoma ili wapate mambo ya kisasa yanayoendana na teknolojia iliyopo ili kuondokana na mazoea.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.Box 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 023 2440149
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2022 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.