TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) leo tarehe 1 Mei, 2023 imeungana na Watanzania kote nchini kusherekea Siku ya Wafanyakazi Duniani, maarufu kama Mei Mosi.
Sherehe hizo ambazo Kimkoa zimefanyika katika Halmashauri ya Chalinze zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya na Mkoa wa Pwani wakiongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kanali Joseph Kolombo, Mkuu wa Wilaya ya Kibiti ambaye ndiye alikua mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanaongozwa na Kauli Mbiu isemayo "Mishahara Bora na Ajira za Staha ni Nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi, Wakati ni Sasa."
Mhe. Kolombo amesisitiza kuwa Siku ya Mei Mosi ni muhimu kwa watumishi wote duniani, kwani ni siku inayotukumbusha wajibu wetu wa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, kwa umoja, ufanisi na kwa haki.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) tawi la TaSUBa, Bw. Gwakisa Charles amesema TaSUBa imeungana na wafanyakazi wa taasisi nyingine kwenye maadhimisho hayo ikiwa ni njia ya kutambua mchango wa watumishi kwenye utekelezaji wa majukumu yao.
Kitaifa Sherehe za Mei Mosi mwaka huu zimefanyika Mkoani Morogoro ambapo mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.Box 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 023 2440149
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2022 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.