Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa amesema Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ni bidhaa ya kiuchumi kwa wakazi wa mji huo na amewataka kulitumia kwa kukuza uchumi wao na kuitangaza Bagamoyo.
Msigwa ameyasema hayo Oktoba 26, 2024 alipokuwa mgeni rasmi wakati wa kilele cha Tamasha hilo lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.
Msigwa amewataka wakazi wa Bagamoyo na maeneo ya jirani kutanua huduma za makazi, chakula, mavazi, malazi, usafiri, bidhaa za kitamaduni na sanaa ili kukidhi mahitaji ya wageni na washiriki wa Tamasha hilo kubwa linalofanyika kila mwaka.
Katika hatua nyingine, Msigwa amesema kuwa Wizara itaongeza bajeti ya Tamasha la 44 mwakani ili kutimiza lengo la kufanyika kwa siku saba huku akiagiza kuwa na wasanii wakubwa wa kutumbuiza kwa siku zote za tamasha.
Naye Mkuu wa Taasisi hiyo, Dkt. Herbert Makoye amewashukuru washiriki na wananchi wote waliojitokeza kuhudhuria shughuli hiyo na kuwaahidi kuboresha zaidi katika Tamasha linalofuata la mwakani.
Tamasha hili la Sanaa na Utamaduni, hufanyika kila mwaka katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ambapo hukutanisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Tamasha hili hulenga kukuza vipaji, kuuenzi na kuutunza na kurithisha Utamaduni wetu kwa vizazi vijavyo, kutangaza utalii wa mji wa Bagamoyo, pia kutoa ajira kwa wasanii wa nyanja mbalimbali nchini.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.