WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa Tamasha la 43 la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo limeshirikisha Nchi 9 Duniani pia limetoa fursa za ajira na biashara kwa wananchi wa Bagamoyo na washiriki wa Tamasha hilo.
Mhe. Dkt Ndumbaro ameyasema hayo wakati akizindua rasmi Tamasha la 43 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Oktoba 23, 2024 ambapo amezitaja mingoni mwa nchi ambazo zimeshawasili ni pamoja na Comoro, Africa ya Kusini na Zambia, ambapo nchi zingine zitawasili leo. Mhe. Dkt Ndumbaro amesema Tamasha hilo linatoa fursa kwa wakazi wa Bagamoyo ambao wataweza kufanya biashara pamoja na kuonyesha bidhaa zao ili waweze kunufaika kiuchumi.
Katika hatua nyingine Dkt. Ndumbaro ameagiza Tamasha hilo kufanyika kwa siku 7 kuanzia mwakani badala ya siku 4 kama ambavyo limefanyika sasa lengo likiwa ni kuendelea kutoa fursa ya kuitangaza Bagamoyo na Nchi kwa ujumla katika nyanja za kijamii, kiuchumi pia kujitangaza Kimataifa.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.