Koplo Frank Suddah ambae ni mmoja wa wanafunzi kutoka Shule ya Kijeshi ya Mafunzo ya Muziki na Sanaa za Maonesho akishashmbulia jukwaa wakati wanafunzi na waalimu kutoka Shule hiyo ya kijeshi walipotembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Mei 15, 2026 kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu.Katika ziara hiyo, wanafunzi wa TaSUBa walipata fursa ya kuonyesha vipaji na umahiri wao katika nyanja mbalimbali za sanaa ikiwemo ngoma, sarakasi na muziki. Aidha, burudani mbalimbali zilizotolewa zilionesha kiwango cha juu cha ubunifu, nidhamu na uwezo mkubwa wa vijana hao katika kushambulia jukwaa na kuwaburudisha watazamaji.
Mkufunzi wa ngoma kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Bi. Beatrice Taisamo, amesema taaluma ya ngoma ina mchango mkubwa katika maendeleo ya wasanii na jamii kwa ujumla. Ameeleza kuwa ngoma si burudani pekee, bali ni taaluma inayoweza kumpatia mtu ajira, kipato na heshima katika jamii.Bi. Beatrice amesema kupitia mafunzo ya ngoma, wasanii hupata ujuzi wa kitaalamu unaowasaidia kufanya kazi kwa ubunifu na kujiamini zaidi wanapokuwa jukwaani. Pia ameeleza kuwa taaluma hiyo huwasaidia vijana kutumia vipaji vyao kwa njia sahihi na kujiepusha na vitendo visivyofaa katika jamii.Aidha, amesema wasanii wengi waliopitia mafunzo ya ngoma wamefanikiwa kujipatia ajira ndani na nje ya nchi kupitia vikundi vya sanaa, maonesho mbalimbali pamoja na kushiriki katika matamasha ya kimataifa. Ameongeza kuwa elimu ya sanaa huwapa wasanii uwezo wa kuelewa utamaduni wao na kuutangaza kwa vizazi vya sasa na vijavyo.Bi. Beatrice amewahimiza vijana wenye vipaji vya sanaa kujitokeza na kujiunga na TaSUBa ili kupata elimu na mafunzo yatakayowasaidia kufikia ndoto zao na kuwa wataalamu wa sanaa ya ngoma.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.