NAIBU Waziri wa Habari, Utamadu,ni Sanaa na Michezo mheshimiwa Juliana Shonza, amewataka wahitimu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa) kutumia taaluma waliyoipata kuongeza ari ya utendaji kazi za sanaa huko waendako kufanya kazi katika nchi yetu na hata nje ya nchi.
Mheshimiwa shonza ameyasema hayo katika mahafali ya 29 ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo yaliyofanyika leo ,wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
“Utendaji wenu wa kazi za sanaa utapimwa siyo kwa kutazama matokeo yenu ya mitihani ambayo mmekwisha ifanya na kufaulu bali utapimwa kwa shughuli za sanaa mtakazo kuwa mkizifanya.”alisema Shonza
Naye mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Makoye amesema kuwa anaamini wahitimu waliotunukiwa vyeti vya stashahada na astashahada ,wameatayarishwa kikamilifu katika taaluma zao, kwa hiyo wana ujuzi, uelewa na uwezo wa kufanya mahali popote duniani kwa fani hiyo na ngazi husika.
Katika mahafali hayo ya 29,jumla ya wahitimu 118 wamehitimu astashahada na stashahada katika fani ya sanaa za maonyesho na ufundi,uzalishaji wa sauti na muziki pamoja na uzalishaji filamu na picha jongevu
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.Box 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 023 2440149
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2020 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo . All rights reserved.