MTENDAJI Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye, amelishukuru shirika la maendeleo la Korea (KOICA), kwa kuwezesha kuleta mtaalamu wa muziki kutoka Korea Profesa Heerack Park kufundisha muziki kwa kipindi cha miaka mitatu kwa wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo.
Akizungumz wakati wa hafla fupi ya kumuaga profesa Park iliyofanyika TaSUBa hivi karibuni Dkt.Makoye amesema kuwa uwepo wa profesa Park umekuwa wa manufaa sana kwa TaSUBa kwani ameweza kuchangia maendelea ya sehemu ya muziki kwa kufundisha wanafunzi lakini pia kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya sanaa ikiwemo tamasha la kimataifa la sanaa na utamadunio ,hivyo ameiomba KOICA kuendelea kuleta wataalamu mbalimbali wa sanaa kutoa Korea ili kuweza kubadilishana uzoefu na wataalamu wa TaSUBa katika maeneo mbalimbali yanayohusu sanaa.
Kwa upande wake profesa Park ameshukuru TaSUBa na watumishi wote kwa ujumla kwa namna walivyompa shirikiano katika kipindi chote cha miaka mitatu aliyokaa TaSUBa.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.Box 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 023 2440149
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2020 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo . All rights reserved.