MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na igizo lililofanywa na kikundi cha Sanaa cha Bagamoyo Players cha Taasisi ya sanaa na utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwenye uzinduzi wa Tamasha la urithi lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.
Mama Samia ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, katika hotuba yake ya ufunguzi alisema kuwa amefurahishwa na ujumbe wa igizo hilo lililohamasisha umuhimu wa shirikiano maana huo ndio urithi wetu watanzania.
Nae mtunzi na mongozaji wa igizo hilo Mwalimu Haji Maeda alisema kuwa wameamua kutumia uhusika wa mti na viungo vyake ili konyesha namna watanzania tunatakiwa kuishi kwa kushirikiana kwa ajili ya maendeleo yetu na taifa kwa ujumla.
Igizo hilo la Bagamoyo players lilikuwa linaelezea maswahibu ya mti katika farakano ambapo viungo vya mti vinafarakana na kutengana kila kimoja peke yake ambapo shina,mzizi,matawi matunda na majani vinatengana lakini baadaye vinakuja kuona hakuna kiungo kinachoweza kusimama peke yake hivyo vinaungana tena na kurudisha uhai wa mti.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.Box 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 023 2440149
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2020 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo . All rights reserved.