Balozi wa Japan nchini Tanzania Mh.Shinishi Goto ametembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) lengo ikiwa ni kujionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na Taasisi hiyo ambayo ni kituo chenye ubora uliotukuka Afrika mashariki, katika utoaji wa Mafunzo ya Sanaa na Utamaduni.
Akizungumza katika ziara hiyo Balozi shinishi alisema kuwa lengo la ziara yake ni kuendelea kudumisha na kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya TaSUBa na nchi ya Japan.
Akiwa TaSUBa Balozi Shinishi ameona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi na namna mafunzo yanavyotolewa pamoja na vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na Taasisi katika kutoa mafunzo,lakini pia alipata nafasi ya kuangalia onyesho maalumu la Ngoma na Muziki wa asili lililofanywa na wanachuo pamoja na Wakufunzi wa TaSUBa.
Naye Mkuu wa Chuo wa TaSUBa Dkt.Herbert Makoye alimshukuru Balozi Shinishi Goto kwa kutembelea TaSUBa , lakini pia alimkaribisha kuhudhuria Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo litakalofanyika Mwezi Oktoba mwaka huu.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.Box 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 023 2440149
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2020 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo . All rights reserved.