Mwanzo | Wasiliana nasi | Ingia
   English | Kiswahili
 
 • Kuhusu Chuo

  Historia

  Kati ya mwaka 1963 na 1980 serikali ya Tanzania iliithibitisha kampuni ya kitaifa ya sanaa za maonyesho, miongoni mwa kazi zake ilikuwa ni:

  • Kukuza umoja wa kitaifa kwa kutumia ngoma za kiasili na muziki wa kiasili ya kitanzania.
  • Kuendeleza mbinu mpya na za kisasa katika sanaa za maigizo na sarakasi.
  • Kutembelea sehemu mbalimbali ili kuelimisha jamii kwa kutumia maonyesho.

  Matatizo ya nchi kiuchumi na marekebisho ya mpango wa kimuundo katika miaka ya themanini,iligundulika/kufamika kwamba kampuni haina uwezo kifedha wa kujiendesha na kutimiza wajibu wake.Pia ilionekana kuwa ni muhimu kwa serikali kuongeza nguvu katika maendeleo ya mpango wa mafunzo ili kuwawezesha wasanii waliojumuishwa katika kazi kwa vitendo kuboresha ujuzi wao kisanaa.Kampuni ilikoma na wasanii wake walipewa kazi nyingine katika kuhudumia jamii.

  Badala ya kampuni hiyo,Chuo cha sanaa Bagamoyo kilianzishwa mnamo mwaka 1981,kwa malengo yafuatayo:

  • Kutoa taaluma ya sanaa kiwango cha Stashahada ili kupata ujira na kujiajiri.
  • Kutoa kozi fupi kwa wasanii wenyeji na wageni(toka nje ya nchi)wanaotaka kukuza uwezo/ujuzi wao kisanaa.
  • Kuwafundisha viongozi na watawala katika sanaa kwa ajili ya jumuiya,watu binafsi na mashirika yasiyo ya kibiashara.
  • Kukuza sanaa kwa njia ya utafiti,kuweka kumbukumbu, na kufanya majaribio mbalimbali.
  • Kutoa huduma ya ushauri kwa taasisi, na mtu mmoja mmoja wanaohusika na sanaa.

  DIRA

  Dira ya TaSUBa ni kuwa kituo cha Sanaa na Utamaduni cha ubora uliotukuka barani Afrika katika utoaji wa mafunzo, utafiti, Ushauri wa kitaalamu na uzalishaji wa kazi mbali mbali za sanaa na utamaduni.

  DHIMA

  • Kutoa mafunzo ya kiwango cha hali ya juu ya Sanaa na Utamaduni katika fani za Ngoma, Tamthiliya, Muziki, Sanaa za Ufundi, Ufundi wa jukwaa, Technolojia ya Habari na Mawasiliano, Utafiti na Uongozi wa shughuli za Sanaa na Utamaduni.
  • Kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu wa Sanaa na Utamaduni.
  • Kuzalisha kazi za Sanaa na Utamaduni zilizo katika kiwango cha hali ya juu cha ubora.
Juu
 © [TaSUBa] :::::Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo