Yafuatayo ni majina ya waliochaguliwa kujiunga na chuo muhula wa Aprili 2018 kwa ngazi ya cheti NTA 4,wanatakiwa kuripoti chuoni kuanzia tarehe 10-24 April 2018 kwa ajili ya udahili na kuanza masomo. wafike na Nakala ya Vyeti vya kidato cha Nne.
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo inapenda kuwakaribisha wasanii na vikundi vya sanaa kwa ujumla kuomba kushiriki kwa kufanya maonyesho katika tamasha la 37 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambalo litafanyika katika viwanja vya taasisi (TaSUBa – Bagamoyo) kuanzia tarehe 20 hadi 27 Oktoba 2018.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (Zamani Chuo cha Sanaa Bagamoyo) anakaribisha maombi ya kujiunga na Chuo kwa kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) katika fani zifuatazo. i. Sanaa za Maonyesho na Ufundi (Performing and Visual Arts) - Muziki, Ngoma, Uigizaji, Sarakasi, Ufundi wa Jukwaa (Stage Technology) na Sanaa za Ufundi (Fine Art). ii. Picha Jongevu (Film and TV Production) - Uchukuaji wa Video (Video Shooting), Kuhariri Video (Video Editing), Kuongoza Filamu (Film Directing) na Uandishi Miswada ya Filamu (Script Writing). iii. Uzalishaji wa Muziki na Sauti (Music and Sound Production) - Kurekodi Sauti (Sound Recording), Kurekodi Muziki (Music Recording), Uzalishaji wa Muziki (Music Production) na Usimamizi wa Studio (Studio Management).
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa)imefanya mkutano na wadau wa Sanaa ambao ni Wasanii,Wakufunzi Wastaafu wa TaSUBa, waliowahi kusoma TaSUBa pamoja na Viongozi wengine kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo