29 Sep 2016

TAMASHA LA 35 LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO LAZINDULIWA

NAIBU Waziri wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Annastazia Wambura amewataka vijana kutumia fursa ya Sanaa na Utamaduni ili kujipatia ajira kwa ustawi wa Maisha yao. Bibi Wambura ameyasema hayo mjini Bagamoyo,wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 35 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo,lililoandaliwa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa),lenye kauli mbiu isemayo Sanaa na Utamaduni kwa maendeleo ya Vijana. “Binafsi niwapongeze waliopendekeza kauli mbiu hii kwa sababu imekuja wakati muafaka ambapo Serikali ya awamu ya tano ina Ajenda mahususi ya kuhakikisha kuwa Vijana wa nchi hii wanatumia fursa zote zilizopo kujipatia ajira kwa ustawi wa maisha yao.”alisema Bibi Wambura. Aliongeza kuwa “Tasnia za Sanaa na Utamaduni zina fursa nyingi sana ambazo vijana wanaweza kuzitumia kujipatia ajira na hivyo kuleta tija katika maisha yao na jamii kwa ujumla. Tasnia za sanaa na utamaduni zinatoa fursa kwa vijana kutumia vipaji vyao kubuni sanaa mbalimbali ambazo mbali na kutoa ajira na kuongeza kipato, pia zinasaidia kutangaza utamaduni na sanaa za jamii ya Watanzania ndani na nje ya nchi yetu.” Naye mtendaji mkuu wa TaSUBa DKT.Herbert Makoye,alisema kuwa Tamasha hufanyika kila mwaka tangu kuanzishwa kwake mwaka 1982 na mwaka huu linafanyika kwa mara ya 35,likiwa na malengo ya Kuonyesha kazi mbalimbali za sanaa kwa wananchi wa Bagamoyo na Maeneo yanayozunguka kama njia ya kupima kiwango cha usanii kilichofikiwa katika mwaka,Kuelimisha jamii kwa kutumia njia mbalimbali za sanaa na Kuburudisha jamii. “Tamasha linahusisha sanaa za maonyesho yaani Ngoma za asili,sarakali,maigizo na Muziki pamoja na Maonyesho ya sanaa za ufundi na warsha mbalimbali litafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 26 septemba hadi tarehe 2 oktoba”alisema Makoye.

26 Sep 2016

TANGAZO LA MAHAFALI

Mahafali ya 27 ya TaSUBa yatafanyika Tarehe 1 Oktoba 2016 Jumamosi saa 3:00 asubuhi. Wahusika ni wanafunzi waliohitimu mafunzo ya Stashahada Juni 2016 na Cheti miaka II waliohitimu 2015. Wote mnakaribishwa.

26 Sep 2016

Tamasha la 35 la sanaa na Utamaduni Bagamoyo kuanza kutimua vumbi hii leo!!!

Kwenye jukwaa hili zitapigwa ngoma,sarakasi,maigizo na miziki italia,leo ndio ufunguzi wa tamasha la 35 la sanaa na Utamaduni Bagamoyo,njoo ule chakula cha asili huku akifurahia ala za muziki wa asili na wa kisasa,huku ukifurahia mandhari murua ya Bagamoyo yetu

08 Sep 2016

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO MWAKA WA MASOMO 2016-2017 TaSUBa

Unatakiwa kuripoti Chuoni tarehe 13/09/2016,tayari kwa kuanza masomo.

17 Aug 2016

Karibuni sana katika Tamasha la 35 TaSUBa Bagamoyo Tanzania!!!

Karibuni wageni wote kutoka ndani na nje ya Tanzania!!!

10 Aug 2016

TANGAZO KWA WALIOOMBA KUJIUNGA NA KOZI NTA 4&5 TaSUBa

Uongozi unapenda kuwajulisha kwamba mchakato wa kuchaguliwa kujiunga na masomo tajwa hapo juu bado haujakamilika kulingana na taratibu za NACTE. Aidha NACTE wameongeza muda wa kuomba nafasi za masomo mwisho tarehe 13/08/2016,baada ya hapo majina ya waliochaguliwa yatatolewa,hivyo vuteni subira. UTAWALA

02 Aug 2016

MATANGAZO MUHIMU KWA WANAFUNZI WOTE WA TaSUBa(CHETI MIAKA II,NTA 4,5 & 6)

Unaombwa usome matangazo hayo kwa makini na kufuata maagizo!!!!

27 Jul 2016

TANGAZO MUHIMU kwa Wanafunzi

1.Mtihani maalumu wa marudio kwa kozi za NTA level 4,5,&6 itafanyika kuanzia tarehe 1/8/2016 Angalizo: i)Angalia ratiba ya mtihani na zingatia tarehe na muda wa mtihani wako.Mtahiniwa anatakiwa kuripoti ofisi ya taaluma saa 2:00 asubuhi siku ya mtihani wake kwa usajili. ii)Malipo yote ya mitihani maalumu (Special exams) yafanyike kupitia taratibu za Taasisi. Malipo yote yalipwe bank na kukabidhi Pay slip Ofisi ya Uhasibu kabla ya siku ya mtihani.Kupitia NMB Ankaunti namba: 2101100012 Jina la Ankaunti:Utawala Chuo cha Sanaa 2.Matokeo ya jumla ya Diploma(PAT&PAD,MST&MSD,MET&MED), na vyeti vya wahitimu vitatolewa vyote kwa wakati moja siku ya Mahafali tarehe 1/10/2016. Angalizo: Endapo mhitimu hakuacha picha, basi aiwasilishe mara moja Ofisi ya Taaluma. 3.Matokeo ya cheti miaka miwili yatatolewa baada ya bodi kutoa idhini ya kuyatangaza.