19 Jun 2017

WITO KWA WASANII NA VIKUNDI KUSHIRIKI KATIKA TAMASHA LA 36 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO KUANZIA TAREHE 23 HADI 30 SEPTEMBA 2017

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo inapenda kuwakaribisha wasanii na vikundi vya sanaa kwa ujumla kuomba kushiriki kwa kufanya maonyesho katika tamasha la 36 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambalo litafanyika katika viwanja vya taasisi (TaSUBa – Bagamoyo) kuanzia tarehe 23 hadi 30 Septemba 2017. Tamasha hili limekuwa na malengo mbalimbali kama vile kuendeleza na kudumisha utamaduni wa Mtanzania, kubadilishana uzoefu na kujifunza kutoka kwa wasanii na vikundi vya Tanzania na mataifa mengine kupitia warsha na maonyesho mbalimbali.

16 May 2017

TANGAZO LA MASOMO MWAKA 2017-2018

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (Zamani Chuo cha Sanaa Bagamoyo) anakaribisha maombi ya kujiunga na Chuo kwa kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma)

29 Apr 2017

Naibu spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson azindua mafunzo maalumu ya Sanaa kwa vijana 27 TaSUBa

Naibu spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson, amewataka wasanii vijana wanaojihusisha na uchezaji wa ngoma za asili kujiunga na Taasisi ya sanaa na utamaduni bagamoyo (TaSUBa )ili wapate mafunzo yatakayowawezesha kufanya shughuli zao kwa Tija . Dkt Tulia ametoa wito huo leo alipokuwa akizindua mafunzo maalumu ya Sanaa kwa vijana 27 kutoka wilaya za Rungwe, Busokelo na Kyela, mkoa wa Mbeya yaliyogharamiwa na Taasisi ya Tulia Trust.N

21 Apr 2017

Ubalozi wa Denmark Nchini Tanzania wafanya makabidhiano ya Vifaa vya Muziki na TaSUBa

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa Na Michezo ,Bibi Nuru Millao ameishukuru Serikari ya Denmark kwa kuwezesha kupatikana kwa vifaa vya kufundishia na kujifunzia Muziki kwa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa). Bi Milao alitoa shukrani hizo leo,wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa TaSUBa uliopo Wilayani Bagamoyo,Mkoa wa pwani ambapo balozi wa Denmark Mh.Einar Herbogard Jensen alikabidhi vifaa vya kufundishia kwa awamu ya pili ambavyo ni kompyuta pamoja na vifaa vya kuhifadhia vyombo vya Muziki,vilivyotolewa na serikali ya Denmark.

04 Apr 2017

WAZIRI wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe (MB)ametembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)

WAZIRI wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe (MB)ametembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kuzindua vifaa vya kufundishia vilivyonunuliwa kwa pesa ya maendeleo iliyotolewa na serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17. Akiwa TaSUBa dkt.Mwakyembe amesema kuwa uhai wa sanaa na utamaduni wa Mtanzania unategemea sana uwepo wa Taasisi ya Sanaa na utamaduni Bagamoyo ambayo ni kituo chenye ubora uliotukuka Afrika mashariki katika kutoa mafunzo ya sanaa na utamaduni.

17 Mar 2017

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii yatembelea TaSUBa

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ikiongozwa na mwenyekiti wake Mh. Peter Serukamba yatembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) leo tarehe 17/03/2017 kuangalia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. Kamati hiyo ilipokelewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa na Naibu Waziri wake Anastazia Wambura.

04 Mar 2017

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)imetoa mafunzo juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya na Mihadarati kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti boys.

27 Feb 2017

TANGAZO LA ZABUNI YA VIFAA VYA STUDIO

23 Feb 2017

PRACTICAL AND THEORY SPECIAL/ SUPPLIMENTARY EXAMINATION 27/02/2017 – 03/03/2017 FIRST AND SECOND AND THIRD YEAR 2016/2017 (SEMESTER I, III &V)

10 Feb 2017

Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Al-haramain wapewa Mafunzo ya siku moja TaSUBa

JUMLA ya wanachuo mia moja na ishirini (120) kutoka chuo cha Ualimu cha Alharamain cha jijini Dar es salaam,wamepatiwa mafunzo juu ya mada isemayo Sanaa ni ajira katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa).

09 Feb 2017

MATOKEO YA MITIHANI YA DECEMBER 2016

TaSUBa inapenda kuwatangazia Matokeo ya Mitihani yote iliyofanyika Mwezi December 2016 kwa mwaka wa Kwanza,pili na tatu.(NTA LEVEL 4,5,6) Hivyo unaweza kuyatazama hapa kwenye Tovuti yetu.

09 Feb 2017

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Natalia Zukerman afanya Onesho TaSUBA

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)imekuwa mwenyeji wa onesho la Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Bi.Natalia Zukerman aliyeambatana na Bi. Mona Tavakoli pamoja na Chaska potter. Onesho hilo la siku moja lilifanyika jana tarehe 08/02/2017katika ukumbi mkubwa wa onesho wa TaSUBa,lilidhaminiwa na ubalozi wa marekani nchini Tanzania.akiongea wakati wa ufunguzi wa maonyesho ,Afisa kutoka ubalozi wa Marekani anayeshughulikia mambo ya Utamaduni,alisema kuwa onyesho hilo lina lenga kudumisha mashirikiano kati ya Tanzania na Marekani ,pamoja na kubadilishana uzoefu wa mambo ya kiutamaduni.

05 Dec 2016

TaSUBa yawanoa Maafisa Utamaduni Tanzania juu Urithi wa Utamaduni unaoshikika na usioshikika katika kuchangia pato la Halmashauri

MAAFISA Utamaduni kutoka Halmashauri mbalimbali za Wilaya,Miji,Manispaa na Majiji wamehitimu mafunzo ya siku tano kuanzia Tarehe28 Novemba 2016 hadi Decemba 02,2016 juu ya Urithi wa Utamaduni unaoshikika na usioshikika katika kuchangia pato la Halmashauri husika,yaliyotolewa katika Taasisi ya sanaa na utamaduni Bagamoyo(TaSUBa),iliyopo Wilayani Bagamoyo,Mkoani Pwani.

29 Sep 2016

TAMASHA LA 35 LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO LAZINDULIWA

NAIBU Waziri wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Annastazia Wambura amewataka vijana kutumia fursa ya Sanaa na Utamaduni ili kujipatia ajira kwa ustawi wa Maisha yao. Bibi Wambura ameyasema hayo mjini Bagamoyo,wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 35 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo,lililoandaliwa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa),lenye kauli mbiu isemayo Sanaa na Utamaduni kwa maendeleo ya Vijana. “Binafsi niwapongeze waliopendekeza kauli mbiu hii kwa sababu imekuja wakati muafaka ambapo Serikali ya awamu ya tano ina Ajenda mahususi ya kuhakikisha kuwa Vijana wa nchi hii wanatumia fursa zote zilizopo kujipatia ajira kwa ustawi wa maisha yao.”alisema Bibi Wambura. Aliongeza kuwa “Tasnia za Sanaa na Utamaduni zina fursa nyingi sana ambazo vijana wanaweza kuzitumia kujipatia ajira na hivyo kuleta tija katika maisha yao na jamii kwa ujumla. Tasnia za sanaa na utamaduni zinatoa fursa kwa vijana kutumia vipaji vyao kubuni sanaa mbalimbali ambazo mbali na kutoa ajira na kuongeza kipato, pia zinasaidia kutangaza utamaduni na sanaa za jamii ya Watanzania ndani na nje ya nchi yetu.” Naye mtendaji mkuu wa TaSUBa DKT.Herbert Makoye,alisema kuwa Tamasha hufanyika kila mwaka tangu kuanzishwa kwake mwaka 1982 na mwaka huu linafanyika kwa mara ya 35,likiwa na malengo ya Kuonyesha kazi mbalimbali za sanaa kwa wananchi wa Bagamoyo na Maeneo yanayozunguka kama njia ya kupima kiwango cha usanii kilichofikiwa katika mwaka,Kuelimisha jamii kwa kutumia njia mbalimbali za sanaa na Kuburudisha jamii. “Tamasha linahusisha sanaa za maonyesho yaani Ngoma za asili,sarakali,maigizo na Muziki pamoja na Maonyesho ya sanaa za ufundi na warsha mbalimbali litafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 26 septemba hadi tarehe 2 oktoba”alisema Makoye.

26 Sep 2016

TANGAZO LA MAHAFALI

Mahafali ya 27 ya TaSUBa yatafanyika Tarehe 1 Oktoba 2016 Jumamosi saa 3:00 asubuhi. Wahusika ni wanafunzi waliohitimu mafunzo ya Stashahada Juni 2016 na Cheti miaka II waliohitimu 2015. Wote mnakaribishwa.

26 Sep 2016

Tamasha la 35 la sanaa na Utamaduni Bagamoyo kuanza kutimua vumbi hii leo!!!

Kwenye jukwaa hili zitapigwa ngoma,sarakasi,maigizo na miziki italia,leo ndio ufunguzi wa tamasha la 35 la sanaa na Utamaduni Bagamoyo,njoo ule chakula cha asili huku akifurahia ala za muziki wa asili na wa kisasa,huku ukifurahia mandhari murua ya Bagamoyo yetu

08 Sep 2016

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO MWAKA WA MASOMO 2016-2017 TaSUBa

Unatakiwa kuripoti Chuoni tarehe 13/09/2016,tayari kwa kuanza masomo.

17 Aug 2016

Karibuni sana katika Tamasha la 35 TaSUBa Bagamoyo Tanzania!!!

Karibuni wageni wote kutoka ndani na nje ya Tanzania!!!

10 Aug 2016

TANGAZO KWA WALIOOMBA KUJIUNGA NA KOZI NTA 4&5 TaSUBa

Uongozi unapenda kuwajulisha kwamba mchakato wa kuchaguliwa kujiunga na masomo tajwa hapo juu bado haujakamilika kulingana na taratibu za NACTE. Aidha NACTE wameongeza muda wa kuomba nafasi za masomo mwisho tarehe 13/08/2016,baada ya hapo majina ya waliochaguliwa yatatolewa,hivyo vuteni subira. UTAWALA

02 Aug 2016

MATANGAZO MUHIMU KWA WANAFUNZI WOTE WA TaSUBa(CHETI MIAKA II,NTA 4,5 & 6)

Unaombwa usome matangazo hayo kwa makini na kufuata maagizo!!!!

27 Jul 2016

TANGAZO MUHIMU kwa Wanafunzi

1.Mtihani maalumu wa marudio kwa kozi za NTA level 4,5,&6 itafanyika kuanzia tarehe 1/8/2016 Angalizo: i)Angalia ratiba ya mtihani na zingatia tarehe na muda wa mtihani wako.Mtahiniwa anatakiwa kuripoti ofisi ya taaluma saa 2:00 asubuhi siku ya mtihani wake kwa usajili. ii)Malipo yote ya mitihani maalumu (Special exams) yafanyike kupitia taratibu za Taasisi. Malipo yote yalipwe bank na kukabidhi Pay slip Ofisi ya Uhasibu kabla ya siku ya mtihani.Kupitia NMB Ankaunti namba: 2101100012 Jina la Ankaunti:Utawala Chuo cha Sanaa 2.Matokeo ya jumla ya Diploma(PAT&PAD,MST&MSD,MET&MED), na vyeti vya wahitimu vitatolewa vyote kwa wakati moja siku ya Mahafali tarehe 1/10/2016. Angalizo: Endapo mhitimu hakuacha picha, basi aiwasilishe mara moja Ofisi ya Taaluma. 3.Matokeo ya cheti miaka miwili yatatolewa baada ya bodi kutoa idhini ya kuyatangaza.