23 Jun 2017

TaSUBa WAPAMBA TAMASHA LA KIGODA CHA MWALIMU NYERERE

Bagamoyo Players ambacho ni kikundi rasmi cha maonyesho cha taasisi ya sanaa na utamaduni bagamoyo (TaSUBa)kimepangatamasha la tisa la Kigoda cha Mwalimu Nyerere kwa kufanya mchezo wa Jukwaani uliobeba maudhui ya kuelezea changamoto mbalimbali zinazolikumba bara la Afrika,kuuona mchezo huo ingia kwenye Link hii https://www.youtube.com/watch?v=HalfqM7Vs6U

19 Jun 2017

WITO KWA WASANII NA VIKUNDI KUSHIRIKI KATIKA TAMASHA LA 36 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO KUANZIA TAREHE 23 HADI 30 SEPTEMBA 2017

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo inapenda kuwakaribisha wasanii na vikundi vya sanaa kwa ujumla kuomba kushiriki kwa kufanya maonyesho katika tamasha la 36 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambalo litafanyika katika viwanja vya taasisi (TaSUBa – Bagamoyo) kuanzia tarehe 23 hadi 30 Septemba 2017. Tamasha hili limekuwa na malengo mbalimbali kama vile kuendeleza na kudumisha utamaduni wa Mtanzania, kubadilishana uzoefu na kujifunza kutoka kwa wasanii na vikundi vya Tanzania na mataifa mengine kupitia warsha na maonyesho mbalimbali.

16 May 2017

TANGAZO LA MASOMO MWAKA 2017-2018

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (Zamani Chuo cha Sanaa Bagamoyo) anakaribisha maombi ya kujiunga na Chuo kwa kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma)