13 Apr 2018

AFRIKA ZINDUKA YA BAGAMOYO PLAYERS YATIKISA KIGODA CHA NYERERE

Mchezo wa kuigiza wa jukwaani unaofahamika kwa jina la Afrika zinduka, umetikisa tamasha la kumi la kigoda cha Mwalimu Nyerere lililoendelea katika ukumbi wa Nkuruma wa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Mchezo huo uliobeba ujumbe wa namna Bara la Afrika linavyoteseka na umasikini mkubwa ile hali lina utajiri mkubwa wa mali asili , ardhi na madini umetungwa , umeongozwa na kuchezwa na Kikundi cha “Bagamoyo Players” cha Taasisi ya Sanaa na utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ili kuchagiza ujumbe wa tamasha la mwaka huu uliosema “wimbi la uporaji wa rasilimali Afrika wanyonge wanajikwamuaje”
 Download Attachment ONESHO KIGODA CHA MWALIMU NYERERE.pdf